HATUA ZA GERD (GASTROESOPHAGEAL REFLUX DISEASE)
Zipo hatua 4 ambazo GERD (kuzid kwa acid tumbon) hupitia,hatua hizo ni kama ifuatavyo:
A .HATUA YA KWANZA (MILD GERD).
Wengi katika watu wanaosumbuliwa na GERD huangukia katika hatua hii ya kwanza ya GERD ambapo tatizo huwa katika hatua za mwanzo sana.
DALILI ZA GERD HATUA YA KWANZA (MILD GERD)
1. Kiungulia
2. Maumivu ya kifua
3. Kuhisi kama kuna vitu vya kunata katika kooni
4. Kucheua chakula au vinywaji
⚫ Katika Hatua hii,mtu anaweza kujitibia kwa kubadili mfumo wake wa maisha kwa kuepuka vyakula na mifumo isiyofaa kutokana na hali yake mfano ajiepushe na Caffeine, pombe,vyakula vyenye mafuta mengi nk. Lakini pia ni rahisi mgonjwa kupona akitumia dawa katika hatua hii ya awali.
B. HATUA YA PILI YA GERD (MODERATE GERD)
Katika hatua hii,watu wenye GERD hupatwa na dalili za GERD mara kadhaa ndani ya wiki na dalili zake hutokea mara kwa mara ukilinganisha na Hatua ya kwanza na dalili huanza kuwa kali kiasi.
DALILI ZA GERD HATUA YA PILI (MODERATE GERD)
1. Kiungulia kikali kiasi
2. Maumivu ya kifua
3. Kuhisi uteute wenye kunata kooni
4. Kucheua chakula au vinywaji
5. Moyo kupaparika (Heart palpation)
⚫ Katika hatua hii,mtu anahitajia matibabu ya dawa pia kumshirikisha daktari kwaajili ya ushauri wa kimatibabu na dawa.
C. HATUA YA TATU YA GERD (SEVERE GERD)
Katika hatua hii, asilimia 15% ya wagonjwa waliopo katika hatua hii hupata dalili za GERD kali mara nyingi zaid kwa wiki au kila siku.
DALILI ZA GERD HATUA YA TATU (SEVERE GERD)
1. Kiungulia kikali
2. Kucheua sana chakula na vinywaji na wakati mwingine kucheua Acid (uchachu)
3. Kuvimba kwa koo(sore throat)
4. Kikohozi kisichoisha
5. Sauti ya kukwaruza
6. Mapigo ya moyo kwenda kasi
7. Wasiwasi uliopita kiasi bila sababu
8. Kuota ndoto za kutisha
9. Kichwa Kuvurugika na kuhisi kuchanganyikiwa
10. Kizunguzungu
11. Maumivu ya kichwa
12. Macho kupungua nguvu ya kuona
13. Maumivu makali ya mgongo
14. Mwili kudhoofika
15. Kuhisi dunia imekutenga
16. Kujisaidia choo kigumu zaidi.
⚫ Katika hatua hii,GERD isipochukuliwa hatua basi kuna hatari ya mtu kupata matatzo makubwa zaid ya kiafya kama vile KANSA YA KOO (EUSOPHAGEAL CANCER).
D. HATUA YA NNE YA GERD (REFLUX-INDUCED PRECANCEROUS LESIONS/ESOPHAGEAL CANCER)
Hatua hii inawakilisha matatzo makubwa zaidi kwa GERD ya muda mrefu na inakadiriwa ya kwamba,asilimia 10% ya wagonjwa wa GERD hufikia hatua hii ikiwa GERD haijadhibitiwa kwa muda mrefu. Hatua hii mgonjwa anaweza kupata Kansa ya koo nk.
DALILI ZA GERD HATUA YA NNE
1. Kiungulia kikali
2. Kucheua vyakula na vinywaji
3. Sauti kukwaruza
4. Kikohozi kikali
5. Chakula kukwama kooni/kunasa koona wakati wa kula.
6. Pamoja na dalili zote zilizopo katika hatua ya 3 ya GERD.
⚫Katika hatua hii mgonjwa anaweza kupata changamoto kama vile esophageal strictures, Barrett’s esophagus na hata KANSA YA KOO (esophageal cancers)
Call: 0758606089
Comments
Post a Comment